Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
--
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa donge
nono la Shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana
kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya
kuwamwagia na kuwadhuru watu tindikali.
Hatua
hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali
nchini.Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo
hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa
kuwafichua watu hao.
“Nimeamua
kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana
kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa
na madhara makubwa,” alisema Kova.
Hivi
karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center, Mfanyabiashara
wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa
ni tindikali.