Wednesday, September 25, 2013

UNAJUA JINSI YA KUTUNZA NGOZI YAKO NA KUTO KUWA NA CHUNUSI USONI?

Ngozi na uso uliotibiwa kwa dawa za kiasili 

IKIWA unapendelea kuwa na ngozi ya kuvutia huna budi kuifuatilia vyema na kuipa matunzo yanayostahili.

Kunywa na kula chakula bora ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia kuwa na ngozi yenye afya siku zote. Lakini ulaji huo, hufanya kazi vizuri zaidi kwa ndani, hivyo si vibaya na wewe ukafanya jitihada za makusudi katika kuhakikisha ngozi yako inakuwa na muonekano mzuri kwa nje.

Katika kuhakikisha hilo linafanyika, unahitaji kuwa na vitu maalumu utakavyotumia kukamilisha azma yako hiyo tena ukiwa nyumbani kwako, na pia bila kutumia gharama kubwa.

Unga wa dengu

Unga wa dengu ni miongoni mwa ‘scrub’ bora kabisa za kiasili. Inasaidia kuboresha ngozi na kuondoa mafuta yaliyoganda katika ngozi hususani ya uso. Kwa kufanya hivyo, inaweza kuifanya ngozi ya uso wako kuwa laini na nyororo tena yenye afya tele.

Unachotakiwa kufanya ni kuchukua vijiko vitatu vya mezani vya unga huo wa dengu na kuchanganya na maji ili kupata rojo zito.

Safisha uso wako vizuri, kisha pakaa mchanganyiko wako kuzunguka uso. Acha mchanganyiko huo ukae usoni kwa muda wa dakika 10 hadi 15. Kisha osha uso wako na maji ya uvuguvugu.

Tango

Sifa kubwa ya tunda hili ni ule uwezo wake wa kuweza kupambana na kuchakaa na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na tabia mbalimbali.

Pia  lina uwezo mkubwa wa kusafisha ngozi hasa ya uso. Hiyo ni kazi moja kati ya nyingi zinazofanywa na tunda hili.
Unachotakiwa kufanya ni kusaga tango moja, kisha kuchuja juisi yake. Chukua pamba na chovya kwenye mchanganyiko wako kisha pakaa usoni. Kaa kwa muda wa dakika 20 hadi 30. Osha uso wako, kisha kausha kwa kitambaa safi na laini.

Ikiwa juisi itakuwa nyingi, unaweza kuihifadhi kwenye jokofu kwa ajili ya matumizi ya siku za baadaye.


Kiini cha yai
Kiini cha yai kina virutubisho muhimu sana kwa ajili ya kuboresha ngozi yako. Kwa kuchanganya kiini cha yai moja na nusu kijiko ya mafuta ya Rose na nusu kijiko ya juisi ya limao, utapata mchanganyiko wa kipekee unaweza kuleta maajabu makubwa katika ngozi yako hususani ya uso.
Unatakiwa kupaka mchanganyiko huo na kukaa nao kwa muda usiopungua dakika 15, kabla ya kuosha maji ya uvuguvugu.

Asali na mtindi

Mchanganyiko wa asali na mtindi unatambulika kama mask bora zaidi hasa katika ngozi kavu. Asali ni unyevunyevu (‘moisturizer’ )wa kiasili wenye matokeo mazuri kuliko zaidi duniani.

Unachotakiwa kufanya ni kuchukua kiasi sawa cha mtindo na asali na kuchangan