Mbunge wa
Nzega-CCM Hamis Kigwangalla Amefanya Mahojiano na Kipindi Cha Makutano
Show Kuhusu Vuguvugu la Urais 2015 Linaloendelea ndani ya CCM
Nakusema;'' Sitompa Kura Mheshimiwa Edward Lowassa.''
Fina Mango na Hamis Kigwangalla baada ya kipindi cha Makutano katika studio za Magic FM.
Add caption |
Mheshimiwa Hamis Kigwangalla akijibu swali kuhusu kugomea urais 2015 ndani ya CCM.
Fina Mango akimsiliza Mheshimiwa Kigwangalla wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi cha Makutano.
Mbunge
wa Nzega-CCM Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa endapo
jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais. Kigwangalla
aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Fina Mango katika
kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani
ya CCM juu ya mgombea urais huku Mheshimiwa Lowassa akiwa kati ya wale
wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.
"Sitompa
kura Mheshimiwa Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba
ninakipenda chama changu na nina hakika chama changu kikija na mgombea
kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye ana historia ya kuhusishwa na mambo
machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema wewe mwenye hapa
tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa
tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema kwamba tunalea ufisadi,
tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili" Alisema Mheshimiwa Kigwangalla
huku akiongezea kuwa Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli.
Akijibu swali kuhusu mitambo ya dowans, Kigwangalla alisema haoni tatizo
la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake.
Katika
mahojiano hayo Mheshimiwa Kigwangalla alitangaza nia yake ya kugombea
urais mwaka 2025 na kuongezea kuwa 2015 anaona bado ni mapema kwake
kwani anaamini watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa
aina gani.
( habari hii ni kwa niaba ya haki ngowi blogspot.com)