MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI AU KABLA YA KUNUNUA KIWANJA CHAKO
Kabla ya kununua kiwanja ni muhimu kujua sababu ya kununua kiwanja unanunua
eneo hilo.Je ni kwa ajili ya shughuli za kilimo, nyumba ya kuishi au biashara, kiwanda etc. Kumbuka kuwa nyumba au ardhi ni hazina hivyo hakikisha na ni sehemu sahihi ya shughuli yako. Kama ni eneo la makazi basi zingatia haya:-
- Hakikisha muuzaji anatoa hati sahihi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.
- Eneo liwe karibu na huduma muhimu kama soko, msikiti au kanisa, shule, stendi ya mabasi, hospitali na huduma nyingine muhim.
- Pia ni vema kuangalia udongo au arthi ya eneo husika kama ni sahihi kwa aina ya shughuli unayotaka kufanya au nyumba unayotaka kujenga.
- Ni vizuri pia kujua kama ni eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi ili kuepuka kuvunjiwa yako.
- Hakikisha ni eneo salama na linalofikika, hapaathiriwi na mafuriko, wala mmomonyoko wa udongo. Pia pasiwe ni karibu na viwanda hatarishi kwa malezi ya watoto
- Je, pana mvuto au mwonekano unaotaka wewe? Je kipo ndani ya bajeti yako?
- Vipi hali ya upatikanaji wa maji na umeme katika eneo hilo?