Jinsi ya kupanga chumba cha mtu mmoja
Vyumba hivi mara nyingi vinakuwa ni vya wastani, hivyo vinatakiwa viwe visafi muda wote kwani hapo ndio chumbani,sebuleni,dining etc. Hutakiwi kujaza vitu vingi chumbani.
Kwanza: angalia ukubwa wa chumba chako.
Pili: Rangi utakayopaka hakikisha itafanya chumba kiwe kikubwa, rangi hizo ni, rangi zilizo angavu (bright) hufanya chumba kiwe kubwa na zilizo poa zinafanya chumba kiwe kidogo.
Tatu: Angalia unahitaji ceiling board(gypsum au ya kawaida) na sakafu ya aina gani, kama ni tiles, ama utaweka carpet, ama cement na kadhalika
Nne: Angalia wingi wa fenicha zako. Vitu muhimu kwa mwenye chumba kimoja ni: kitanda, kabati la nguo, tv na radio, fridge, shoe rack, jiko, kochi dogo hata la mtu 1 na kameza ama stuli inategemea na ukubwa wa chumba. Angalia kama vyote vyaweza kuingia, ila kama haviingii basi, punguza vitu kwa kutumia njia ya 2 na ya 1. Hii ni, mfano kabati la nguo unganisha na shoe rack, meza ya tv tafuta inayoweza kuhifadhi vyombo, radio na tv yenyewe, kitanda sio lazima kiwe kikubwa. Hapa utakuwa umepata nafasi hata ya kupita.
Mwisho: Rembesha chumba chako kwa picha za ukutani chache hata moja ikiwezekana na saa ya ukutani.
Siri ya kuwa na chumba kisafi wakati wote acha kuweka vitu chini ya uvungu, na kila unapoamka tandika kitanda kabla ya kwenda kuoga. Ukiacha nyumba chafu, ukirudi ndio unachoka zaidi? nyumbani kwako ndio sehemu ya kupumzika na kutafakari kuwa kesho inakuwaje na kadhalika.