Monday, June 9, 2014

Muigizaji mkongwe,Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki Dunia






Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku wa jana akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa juzi na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha baba yake huyo "Mzee Small"
mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko nyumbani kwake Tabata mawenzi alipokuwa akiishi katika enzi za uhai wake. 
Kampuni ya Malogo Estate inatoa pole kwa Familia yake
Bwana ametoa,bwana ametwaa
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
CHANZO: GPL